Main Title

source : Parstoday
Jumatano

16 Novemba 2022

17:23:01
1323745

Iran: Ni kichekesho kwa nchi kama Australia kuzungumzia haki za binadamu

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu matamshi ya Waziri Mkuu wa Australia ya kuingilia masuala ya ndani ya Iran na kueleza kuwa, matamshi hayo ya Antony Albanese yametegemea taarifa za uongo.

Nasser Kan'ani Chafi amemtahadharisha Waziri Mkuu huyo wa Australia akisema kuwa, matamshi kama hayo hayasaidii chochote katika juhudi za kuweko uhusiano mzuri baina ya pande mbili.

Kuhusiana na tuhuma za Australia dhidi ya Iran kwamba, inakiuka haki za binadamu, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, kuheshimiana pande mbili na kuzingatia uhalisia wa mambo ndio njia bora kabisa ya kujiepusha na mizozo na mivutano ya kidiplomasia.

Chafi amekosoa vikali hatua ya Antony Albanese, Waziri Mkuu wa Austalia na kutoa mtazamo kuhusiana na masuala ya ndani ya Iran sambamba na hatua yake ya kuwaunga mkono wafanya fujo na waibua machafuko hapa nchini. 

Ameongeza kuwa, nchi kama Australia ambayo yenyewe ina faili chafu la ukiukaji wa haki za binadamu kuanzia kuwaua wahajiri mpaka mauaji yake ya watu 500 raia wa asili wa nchi hiyo katika magereza yake, haina haki wala ustahiki wa kufungua kinywa na kuzungumzia haki za binadamu.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, hatua ya Australia ya kutoa hifadhi kwa makundi ya kigaidi na wapigania kujitenga na kunyamazia kimya shambulio la kigaidi la hivi karibuni dhidi ya Haram ya Shah Cheragh mjini Shiraz hapa Iran ni ishara ya wazi ya unafiki na undumakuwili wa nchi hiyo katika suala la haki za binadamu.

342/