Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

17 Novemba 2022

18:13:30
1324045

Mgogoro wa mafuta Ulaya, wananchi washambulia vituo vya mafuta Ufaransa

Madereva wa vyombo vya usafiri nchini Ufaransa wameshambulia vituo vya mafuta na kusababisha foleni kubwa baada ya bei ya bidhaa hiyo muhimu kupaa vibaya wakati huu wa mgogoro mkubwa wa nishati barani Ulaya.

Televisheni ya Ruptly imeripoti habari hiyo leo na kuongeza kuwa, makumi ya madereva wa magari ya usafiri mjini Paris wamevamia vituo vya mafuta kabla ya serikali ya Emanuel Macron na shirika la Total ambalo ndilo shirika kuu la mafuta nchini Ufaransa kupunguza ruzuku yake ya kufidia bei ya petroli na dizeli. 

Jana bei ya mafuta nchini Ufaransa ilipanda kwani ruzuku iliyokuwa inatolewa na serikali imepungunguzwa kutoka senti 30 hadi senti 10 kwa pipa.

Mgogoro wa Ukraine ni moja ya sababu za kupaa bei ya nishati barani Ulaya

Shirika la mafuta la Total lilikuwa limeweka punguzo la senti 20 katika vituo vyake vya mafuta lakini kuanzia Jumatano, punguzo hilo limeondolewa na kubakia senti 10 tu. 

Baada ya kupunguzwa ruzuku ya mafuta katika nchi ya Ulaya ya Ufaransa, madereva hasa wa magari ya usafiri wamekumbwa na hofu kubwa na Jumanne walivamia vituo vya mafuta ili kujaza magari yao kabla ya kuanza kufanya kazi bei mpya za bidhaa hiyo muhimu sana. 

Magari yalikuwa mengi kiasi kwamba akiba iliyokuwepo kwenye vituo hivyo vya mafuta iliisha katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ya Ulaya ukiwemo mji mkuu Paris na na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Mmoja wa madereva hao amenukuliwa na televisheni hiyo akisema, ni aibu kuiona hali hii. Kila mtu ameamua kujaza mafuta leo kwenye gari yake kwa hofu ya kupanda vibaya bei. 

342/