Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

17 Novemba 2022

18:16:38
1324050

Raisi: Maadui wanataka kuwakatisha tamaa wananchi wa Iran

Rais wa Iran amesema maadui wanafanya juu chini na kula kila aina ya njama kwa lengo la kuwakatisha tamaa wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Rais Ebrahim Raisi amesema hayo leo Alkhamisi katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Jihad ya Maelezo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano hapa Tehran na kuongeza kuwa, nchi za Magharibi zinatumia vyombo vyao vya habari kuchochea moto na fujo na ghasia hapa nchini, kwa kisingizio cha kifo cha Mahsa Amini.

Rais Raisi amebainisha kuwa, Iran hii leo inakabiliwa na vita vya vyombo vya habari, na sharti iandae mbinu na mikakati ya kujibu mapigo.

Amesema utamaduni wa Kiislamu una Jihadi ya kutoa maelezo na ufafanuzi, jambo ambalo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei amekuwa akilisisitizia mara kwa mara.

Rais wa Iran ameeleza kuwa, "kwa mujibu wa Qurani tukufu, wambeya na waongo ni kama wanafiki na makafiri, na kitendo cha waongo na watu wadaku kujaribu kupindisha mitazamo na elimu kwa maslahi yao, kinafanana na cha kinafiki."

Vyombo vya Mghribi

Rais wa Iran ametoa mwito kwa wasomi, wakurugenzi na maafisa wa Uhusiano Mwema kote nchini kutonyamaza kimya, akisisitiza kuwa wanapaswa kuchukua hatua za kukabiliana na vita vya vyombo vya habari dhidi ya taifa hili. 

Sayyid Ebrahim Raisi amesema: Stratejia ya adui ni kukatisha tamaa; Vyombo vya Uhusiano Mwema na vyombo vya habari vinapaswa kueleza 'tunaweza.'

342/