Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

17 Novemba 2022

18:17:19
1324051

Iran na Afrika Kusini zaazimia kuimarisha uhusiano wa pande mbili

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Afrika Kusini wamesisitizia haja ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa nchi hizi mbili katika nyuga tofauti.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian amesema katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Afrika Kusini kwamba, anatumai nchi mbili hizi zitapiga hatua madhubuti za kuimarisha uhusiano wa pande mbili, katika kikao kijacho cha Kamisheni ya Pamoja ya Iran na Afrika Kusini.

Kadhalika mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran ameonya kuhusu matokeo mabaya ya hatua ghalati na mahesabu mabaya ya Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya katika mkutano wa Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Naledi Pandor amekaribisha mpango wa kufanyika kikao cha Kamisheni ya Pamoja kwa kuwashirikisha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi mbili hizi.

Amesema anatumai kuwa, kamisheni hiyo itafanikisha mchakato wa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na Iran na Afrika Kusini katika sekta mbalimbali.

Aidha ametangaza kuunga mkono mazungumzo ya kidiplomasia ya kadhia ya nyuklia, akisisitiza kuwa Afrika Kusini inataraji kuwa pande zote husika kwenye mapatano hayo zitajitolea kufuata njia ya diplomasia, ili mazungumzo hayo yazae matunda na Iran iondolewa vikwazo.

342/