Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

17 Novemba 2022

18:18:18
1324053

Kadhaa watiwa mbaroni kwa kuhusika na shambulio la kigaidi lililoua watu 5 kusini mwa Iran

Vikosi vya usalama vya Iran vimewatia mbaroni watu kadhaa wanaohusishwa na shambulio la kigaidi lililosababisha vifo vya watu sita usiku wa kuamkia leo katika mkoa wa Khuzestan, kusini magharibi mwa nchi.

Ali Dehqani, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Sheria katika mkoa wa Khuzestan amesema vyombo vya usalama nchini vimewatia mbaroni magaidi watatu wakuu ambao walihusika na shambulio hilo la umwagaji damu.

Amesema operesheni kali za kuwasaka na kuwakamata magaidi wengine waliohusika na kitendo hicho cha ugaidi cha jana usiku mkoani Khuzestan inaendelea.

Watu wasiopungua sita wameuawa shahidi huku wengine zaidi ya kumi wakijeruhiwa, baada ya magaidi wawili waliokuwa juu ya pikipiki kuwashambulia kwa risasi raia na maafisa usalama katika mji wa Izeh mkoani Khuzestan, kusini magharibi mwa Iran.

Maafisa usalama wameeleza kuwa, waliouawa shahidi katika hujuma hiyo ya jana usiku ni mtoto wa miaka tisa, mwanamke wa miaka 45 na vijana mabarobaro watatu. Majeruhi wa shambulio hilo wamehamishiwa katika hospitali za kaunti ya Ahvaz.

Ikumbukwe kuwa, gaidi aliyekuwa na silaha nzito alivamia Haram Takatifu ya Shah Cheragh mnamo Oktoba 26 katika mkoa wa kusini wa Fars kabla ya Swala ya Magharibi na kuua wafanyaziara 15 akiwamo mwanamke na watoto wawili na kuwajeruhi wengine 40.

Mashambulio hayo ya kigaidi yanajiri wakati huu ambapo nchi za Magharibi zinaendelea kuchochea moto na fujo na ghasia hapa nchini, kwa kisingizio cha kifo cha mwanamke wa Kiirani, Mahsa Amini kilichotokea katikati ya Septemba.

342/