Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

17 Novemba 2022

18:18:47
1324054

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran: Adui anataka kuvuruga mahusiano ya wananchi

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran ameeleza kuwa adui amekusudia kuvuruga maelewano na maingiliano kati ya matabaka mbalimbali ya wananchi na kwamba, wale wanaotoa madai kuhusu haki za binadamu wao mwenyewe ni wakiukaji wa haki za binadamu.

Alipoulizwa swali na Iran Press pambizoni mwa kikao cha baraza la mawaziri, Ahmad Vahidi Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran ameongeza kuwa: Marekani, utawala wa Kizayuni, Uingereza na Saudi Arabia ni kati ya nchi ambazo zinasimamia kituo cha kuuibuua ghasia na fujo nchini Iran. 

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran aliendelea kubainisha kuwa: "Adui anafanya kila linalowezekana kuvuruga hali ya usalama na kuibua machafuko, kusitisha harakati za kielimu na sayansi hapa nchini, kuvuruga biashara na shughuli za wananchi; hata hivyo ameshindwa kufanikisha malengo yake kutokana na jibu la haraka la idara ya intelijinsia na usalama ya Iran. 

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Ahmad Vahidi ametangaza kukamatwa kwa maafisa wa kijasusi wa Ufaransa na wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) katika ghasia za hivi majuzi na kuongeza kuwa watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani.

Akijibu swali kuhusu kukamatwa kwa watu wa mataifa mengine katika matukio ya hivi majuzi nchini Iran, Vahidi amesema: "Maafisa wa ujasusi wa Ufaransa na wanachama wa ISIS ambao walikamatwa katika ghasia za hivi karibuni wamekabidhiwa kwa Idara ya Mahakama. Amesisitiza kuwa, watu wa mataifa mengine walikamatwa katika ghasia hizo na kwamba baadhi yao walikuwa na nafasi kubwa katika machafuko ya karibuni hapa nchini.

342/