Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

18 Novemba 2022

19:08:27
1324313

Wakazi wa mji wa Izeh, kusini magharibi mwa Iran washiriki maziko ya wahanga wa ugaidi

Wananchi wa mji wa Izeh ulioko kusini magharibi mwa Iran, leo Ijumaa wameshiriki katika maziko ya wahanga wa shambulizi la kigaidi lililotokea jioni ya juzi Jumatano.

Kwa mujibu wa Press TV, maziko hayo yameanza leo Ijumaa asubuhi na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wakazi wa mji huo wakiwemo piaa maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa serikali na jeshi. 

Watu saba, akiwemo mtoto na mwanamke mmoja waliuawa shahidi na wengine kumi kujeruhiwa baada ya watu wawili wenye silaha kuwafyatulia risasi kiholela watu katikati ya mji huo wa mkoa wa Khuzestan, Jumatano jioni.

Waliouawa wametambuliwa kwa majina ya i Reza Shariati, miaka 25, Kian Pir Falak, miaka 9, Ashraf Nikbakht, 45, Abtin Rahmani, miaka 13, Ali Moulai na watu wengine wawili ambao hadi tunapokea habari hii walikuwa bado hawajatambuliwa.

Mkuu wa mahakama ya Khuzestan, Ali Dehghani amesema kuwa wahusika wakuu watatu wa shambulizi hilo la kigaidi wametiwa mbaroni. Aidha amesema, juhudi zinafanywa ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wengine wote wa uhalifu huo wa kutisha.

Maafisa wa usalama katika mkoa wa Khuzestan wa kusini magharibi mwa Iran wamesema kuwa, watu wawili wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki walianza kuwafyatulia ovyo risasi watu na maafisa wa polisi katikati mwa mji huo wa Izeh kwa kutumia silaha za kivita, Jumatano jioni.

Katika tukio jengine lililotokea usiku wa hiyo hiyo Jumatano, magaidi waliokuwa wamepanda pikipiki walishambulia walinzi wa usalama mkoani Isfahan (katikati mwa Iran) na kuua shahidi maafisa watatu na kumjeruhi mtu mmoja. Genge la kigaidi la Daesh (ISIS) ndilo linalotangaza mara kwa mara kuhusika na jinai hizo. Iran imesema itatoa jibu kali kwa wapangaji wakuu wa ukatili huo. 

342/