Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

18 Novemba 2022

19:09:59
1324315

Umwagaji damu huko Esfahan, Khuzestan unatokana na kukata tamaa adui na ugaidi wa vyombo vya habari

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani msururu wa mashambulizi ya kigaidi hivi karibuni katika mikoa ya Khuzesatan na Esfahan, akisema ugaidi huo unatokana na kuchanganyikiwa na kukata tamaa maadui na vile vile ugaidi wa vyombo vya habari unaoendeshwa dhidi ya taifa la Iran.

Akizungumza hapo jana Alhamisi kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi ya ufyatuaji risasi katika miji ya katikati mwa nchi ya Semirom na Malekshahr pamoja na mji wa kusini-magharibi wa Izeh, ambayo yalisababisha raia kadhaa na maafisa wa usalama kuuawa na kujeruhiwa, Ali Bahadori Jahromi amesema:

"Wale wote waliohadaika na magaidi wa vyombo vya habari wanapaswa kuwajibishwa kutokana na vitendo vyao katika mitaa ya Izeh na Esfahan." Ameongeza kuwa vitendo hivyo vya ugaidi havitapita hivi hivi bila kujibiwa.

Amesema: "Maadui na wale wanaoendesha ugaidi wa vyombo vya habari wanajaribu kutekeleza ajenda zao kwa kueneza propaganda dhidi ya Iran kupitia mbinu tofauti za makelele ya vyombo vya habari na hila ambazo hazieleweki kirahisi, lakini wanaposhindwa kufikia malengo yao na kupoteza matumaini, huamua kutumia ugaidi dhidi ya raia wasio na hatia.”

"Hawajali kuhusu watoto wala wanawake wa Iran", Bahadori Jahromi amesema, na kuongeza kuwa: "Wanapiga nara za kuunga mkono uhuru na wanawake lakini kwa kweli ni wapeperushaji bendera ya vitendo vya ugaidi."

Siku ya Jumatano, takriban watu saba waliuawa kinyama baada ya magaidi kuwafyatulia risasi raia na maafisa wa usalama katika soko lililokuwa limefurika watu huko Izeh katika mkoa wa Khuzestan kusini magharibi mwa nchi.Mtoto wa miaka tisa, mwanamke mwenye umri wa miaka 45, na vijana watatu ni miongoni mwa watu waliouawa shihidi katika tukio hilo la kigaidi. Takriban watu wengine 10 pia walijeruhiwa, wanne kati yao wakiwa katika hali mahututi kufuatia tukio hilo la kinyama.

Wakati huo huo, watu watatu waliuawa na askari usalama wanane kujeruhiwa wakati wa ghasia huko Semirom katika mkoa wa Isfahan katikati mwa nchi. 

Askari wawili wa usalama pia waliuawa na magaidi na wengine wawili kujeruhiwa katika mji wa Malekshahr katika mkoa huo huo wa Isfahan.


342/