Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

18 Novemba 2022

19:12:43
1324318

SEPAH: Ndoto ya adui ya kuigawa vipande vipande Iran kamwe haitoaguka

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesisitiza kuwa, Marekani ina hamu ya kuwaona vijana wa Iran wanauawa mitaani na kuona nyuso za watu zinasinyaa, wananchi wanakasirika na Iran inagawanyika vipande vipande, lakini ndoto hiyo ya kishetani ya adui kamwe haitoaguka kwani Iran ni taifa imara na la muqawama.

Kikao cha mwisho cha Kongamano la Taifa la 6090 la Mashahid wa Qum kilifanyika jana Alkhamisi na kuhudhuriwa na Brigedia Jenerali Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na maelfu ya wananchi waumini, wanamapinduzi na walioshikamana na viongozi wao wa mkoa wa Qum. Kongamano hilo limefanyika kwenye Msikiti Mtukufu wa Jamkaran mjini Qum.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Brigedia Jenerali Salami akisisitiza kuwa, Marekani ina hamu ya kuona barabara za miji ya Iran zimefunikwa na moshi na moto. Anataka kutufanya maskini, mafakiri na vilema. Adui anataka kuhakikisha kuwa hata tunapoumwa tusiwe na dawa za kututibu.

Brigedia Jenerali Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH

 

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH pia amesema: Wanawake wa Kiislamu wanalihesabu vazi la staha la Hijab kuwa ni ngao ya kulinda matukufu, hadhi na heshima yao na kila mwanamke wa Kiislamu, hawezi kuitikia mwito wa kishetani wa adui wa kumtaka asijisitiri vizuri.

Vile vile amesema, tumepata tajiriba na mafunzo mengi katika njia za Jihad na tutaendelea mbele na njia hii tukufu. Ushawishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utaendelea kuwepo. Nguvu za kujihami za askari wetu zitaongezeka. Uchumi wetu utazidi kustawi na tuna imani kuwa Muirani yeyote mwenye fikra huru, awe Muislamu au asiye Muislamu, hayuko tayari kuisababishia madhara nchi yake kwa sababu za kiuchumi.

342/