Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

18 Novemba 2022

19:13:48
1324320

Wapalestina wapata ushindi mwingine Umoja wa Mataifa

Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imepasisha azimio ikitambua haki ya watu wa Palestina ya kuamua hatima yao wenyewe.

Rasimu ya azimio hilo iliwasilishwa na Misri ikishirikiana na serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Umoja wa Mataifa, kwa niaba ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

Azimio hilo limeungwa mkono na nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa, zikiwemo nchi za Umoja wa Ulaya, nchi za Amerika ya Kusini, Asia na Afrika, na linatarajiwa kuwasilishwa kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuidhinishwa katikati ya mwezi ujao wa Desemba.

Nchi 167 zilipiga kura ya kuunga mkono azimio hilo, nchi 5 zimepinga na nchi 7 hazikupiga kura.

Riyad al-Maliki, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amezishukuru nchi zilizopiga kura ya kuunga mkono azimio hilo na kusema: Haki ya kujitawala ndio msingi wa haki zote hususan kwa watu wa Palestina ambao wamekuwa chini ya uvamizi wa kikoloni wa muda mrefu wa utawala wa kibaguzi.

Vilevile amepinga misimamo ya nchi zilizopiga kura ya kulipinga au ambazo hazikupiga kura na kusisitiza kuwa, nchi hizo haziwezi kuendelea kuunga mkono utawala vamizi na jinai zake, na hatua zao zitazidisha kiburi na uhalifu wa utawala huo.

342/