Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

19 Novemba 2022

16:13:08
1324633

Zaidi ya watoto wachanga 80 wanafariki kila siku mara baada ya kuzaliwa nchini Yemen

Afisa wa Wizara ya Afya ya Serikali ya Kitaifa ya Wokovu ya Yemen amesema zaidi ya watoto wachanga 80 hufa kila siku kutokana na ukosefu wa vifaa vya matibabu.

Tangu kuanza kwa vita dhidi ya Yemen mwezi Machi 2015, muungano wa Saudia umeiwekea nchi hiyo mzingiro wa kila upande. Uhaba mkubwa wa fueli nchini Yemen umesababisha kufungwa idara za sekta mbalimbali vikiwemo vituo vya tiba na kupelekea kuzorota hali ya kibinadamu nchini humo.Kwa mujibu wa tovuti ya Al-Khabar Al-Yamani, Najeeb Al-Qabati, mshauri wa Wizara ya Afya ya Serikali ya Kitaifa ya Wokovu ya Yemen, amesema mjini Sana'a kwamba asilimia 39 ya watoto wachanga wanazaliwa kabla ya wakati, hali ambayo imeongezeka sana  ikilinganishwa na kabla ya kuanza vita mnamo 2015.Al Qabati amesisitiza kuwa uvamizi wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudia na utumiaji wake silaha zilizopigwa marufuku ndio sababu kuu ya kuzaliwa watoto njiti nchini Yemen, na akaongeza kuwa mashirika ya kutetea haki za binadamu yameshalaani mara kadhaa utumiaji wa silaha hizo katika vita vya Yemen.Mabomu yaliyopigwa marufuku, yanayotumiwa na muungano wa kijeshi wa Saudia Yemen 

Mshauri wa Wizara ya Afya ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen amebainisha kuwa wizara hiyo inajaribu kuboresha miundomsingi kwa ajili ya watoto katika idara na mikoa na imepanga kuweka vituo vinne vya matunzo ya watoto wanaonyonya katika kila mji na vinane katika kila hospitali kuu.Kuhusiana na suala hilo, Muhammad al-Mansour, Naibu Waziri wa Afya wa serikali ya Sana'a, ameeleza katika mkutano na waandishi wa habari mkoani al-Hudaydah kwamba katika miaka mitano iliyopita, vimerekodiwa vifo 260,000 vilivyotokana na malaria na homa ya dengue, na kwamba kuendelea kwa vita, kuzingirwa Yemen na kushambuliwa kwa mabomu na makombora miundombinu kumechangia sana kuenea maradhi katika nchi hiyo.Maafisa wa Serikali ya Kitaifa ya Wokovu ya Yemen wameshatangaza mara kadhaa kuwa kuzuiliwa meli zinazobeba mafuta kuingia katika bandari ya al-Hudaydah licha ya kuwa na kibali, ni mauaji ya kimbari ya halaiki na kwamba mamilioni ya watoto wagonjwa wako hatarini kufariki dunia kutokana na kuendelea kuzuiliwa dawa kuingizwa nchini humo.../

 

342/