Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

19 Novemba 2022

16:13:45
1324635

Iraq yawatia nguvuni magaidi 15 wa Daesh

Vikosi vya usalama vya Iraq vimewatia mbaroni magaidi 15 wa kundi la Daesh katika mikoa sita ya nchi hiyo.

Mamluki waliosalia wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wangali wanaendesha harakati zao katika mikoa ya Baghdad, Salahuddin, Diyala, Kirkuk, Nainawa na al Anbar huko Iraq. 

Idara ya Usalama wa Taifa ya Iraq jana Ijumaa ilitangaza kuwa, kwa mujibu wa taarifa sahihi za kiintelijinsia na ikiwa katika kukamilisha oparesheni za idara hiyo za kusaka masalia ya magaidi wa kundi la Daesh;  askari wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Iraq wamewatia nguvuni magaidi 15 wa Daesh katika mikoa ya Al Anbar, Nainawa, Salahuddin, Wasit, Kirkuk na Diyala baada ya kupata kibali cha mahakama. 

Taarifa ya Idara ya Usalama wa Taifa ya Iraq imeeleza kuwa, mashambulizi ya vikosi vya Iraq yamepelekea kutekelezwa oparesheni za kuwatia nguvuni magaidi hao wa Daesh kwa mujibu wa kipengee cha nne kuhusu ugaidi. 

Vikosi vya usalama vya Iraq siku zote vimekuwa vikifanya jitihada kubwa za kusaka na kufuatilia mabaki ya magaidi wa kundi la Daesh kote nchini humo ili  kuhakikisha kuwa magaidi hao hawaibuki tena huko Iraq.

342/