Main Title

source : Parstoday
Jumapili

20 Novemba 2022

19:55:36
1324948

Kan'ani: Malengo ya vita vya vyombo vya habari ni kuwasafisha wahalifu washirika wa Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa malengo ya vita vya vyombo vya habari na mashinikizo ya kisiasa ya nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwatakasa wahalifu wenye mfungamano na Marekani.

Nasser Kanani, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter akikumbusha mienendo inayokinzana ya nchi zinazodai kutetea haki za binadamu kuhusiana na jinai na uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel, pamoja na kimya cha mashirika ya kimataifa kuhusiana na mauaji ya ya watoto wa Yemen na kusema: Kuuawa shahidi na kujeruhiwa watoto 8,000 katika vita vya Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Yemen, na hatua ya Israel ya kuwatiwa mbaroni zaidi ya watoto 750, kuuawa shahidi 47 na kujeruhiwa wengine 164 wa Kipalestina kulitokea mwaka huu wa 2022 vimefanywa kwa uungaji mkono wa nchi zinazodai kutetea haki za binadamu na ukimya cha mashirika ya kimataifa.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Yemen limetangaza kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Kibinadamu kwamba muungano wa Saudia umewaua au kuwajeruhi zaidi ya wanawake elfu tano wa Yemen tangu kuanza kwa hujuma na mashambulizi ya nchi hiyo dhidi ya Yemen mwaka 2015.

342/