Main Title

source : Parstoday
Jumapili

20 Novemba 2022

19:57:30
1324950

Rais wa Iran asema Marekani inashindwa kutokana na maendeleo ya Wairani lakini bado haijifunzi kutokana na hilo

Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema Marekani imeshindwa mbele ya maendeleo makubwa yaliyofanywa na taifa la Iran katika kipindi cha miongo minne iliyopita lakini bado haijajifunza kutokana na kushindwa kwake huko.

"Ghadhabu na uadui wa Wamarekani kutokana na maendeleo ya taifa la Iran daima imeendelea bila natija katika miongo minne iliyopita, lakini Wamarekani bado hawajajifunza kutokana na kushindwa kwao," Raisi amesema katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Sayyid Badr Albusaidi mjini Tehran siku ya Jumamosi.

Ameongeza kuwa uadui wa mfumo wa kiburi na kiistikbari unaoongozwa na Marekani kwa taifa la Iran unajulikana kwa wote.

Rais wa Iran kwa mara nyingine tena amesisitiza utayarifu wa Tehran kufikia makubaliano "ya haki" juu ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya 2015, ambayo yanajulikana rasmi kama Mpango Kamili wa Utekelezaji wa


 (JCPOA). Raisi hata hivyo amekosoa muelekeo wa kindumakuwili wa baadhi ya "pande za kikanda na kimataifa" kuhusu suala hili.

Raisi amefafanua nukta hiyo kwa kusema,"Baadhi ya wahusika kikanda na kimataifa wanaendelea kutuma ujumbe kupitia wapatanishi kuwa wanataka kuendelea na ushirikiano, lakini vitendo vyao ni tofauti na maneno yao.

 Unafiki huu bila shaka utawafanya wajute."

Akiashiria uhusiano uliokita mizizi na imara kati ya Tehran na Muscat, Raisi amesema pande zote mbili zimeweza kuboresha uhusiano kiasi cha kuwakatisha tamaa maadui.

Ameongeza kuwa Iran na Oman zimechukua hatua "chanya" katika miezi ya hivi karibuni kutekeleza makubaliano kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman kwa upande wake amepongeza msimamo imara wa Iran kuhusu masuala ya kieneo na kimataifa na kusema Tehran na Muscat zina uhusiano wa kupigiwa mfano.

Albusaidi ametoa wito wa kuboreshwa zaidi uhusiano na Tehran katika nyanja mbalimbali.

Vile vile ameashiria kuunga mkono misimamo ya Iran katika mazungumzo ya kufufua mapatano ya JCPOA na kuondolewa vikwazo na kueleza imani yake kuwa kusimama kidete na ikhlasi ya Tehran kutaleta matokeo mazuri.

Akiongoza ujumbe wa ngazi za juu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman aliwasili Tehran siku ya Jumamosi kwa lengo la kufanya mazungumzo na maafisa wakuu wa Iran. Amefanya duru mbili za mazungumzo na Waziri wa

 Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian na kuhudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

342/