Main Title

source : Parstoday
Jumapili

20 Novemba 2022

19:59:43
1324954

Hamas yalaani hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Syria

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa taarifa akilaani mashambulio ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria.

Shirika rasmi la habari la Syria (SANA) limeripoti kujiri mashambulizi mapya ya anga ya utawala wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya nchi iyo yaliyouwa wanajeshi wanne na kumjeruhi mwingine mmoja.  

Hazim Qassem Msemaji wa harakati ya Hamas ya Palestina amelaani mashambulizi hayo ya Israel dhidi ya Syria na kusisitiza kuwa, mashambulizi ya makombora yaliyotekelezwa Jumamosi asubuhi na utawala wa kizayuni dhidi ya Syria na kuua shahidi wanajeshi kadhaa wa jeshi ya Syria yanadhihirisha sera za uvamizi na uchokozi za utawala huo kwa lengo la kupanua wigo wake wa mashambulizi dhidi ya eneo zima. 

Mashambulizi ya anga ya Israel huko Syria, wanajeshi 4 wameuliwa 

Msemaji wa Hamas ameongeza kuwa, maghasibu wa Kizayuni ni hatari kubwa na ya wazi kwa Umma wa Kiislamu na kwamba hujuma hizo za Wazayuni zitakoma iwapo Umma wote wa Kiislamu utakurubisha pamoja misimamo yao. 

Syria ni moja ya nchi muhimu ya mhimili wa muqawama na yenye nafasi kubwa katika kukabiliana na njama na hatua za muungano wa Marekani-Uzayuni na Saudi Arabia katika eneo la Magharibi mwa Asia. 

342/