Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

21 Novemba 2022

18:54:18
1325174

Mashindano ya Kimataifa ya Qurani yamalizika Moscow, Russia

Duru ya 20 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qurani Tukufu iliyoanza Ijumaa iliyopita katika mji mkuu wa Russia, Moscow imemalizika huku washindi wakitangazwa na kutuzwa.

Raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Mostafa Hosseini ameibuka mshindi wa tatu kwenye mashindano hayo ya dunia yaliyofanyika katika Msitiki wa Jamia jijini Moscow.

Nafasi ya kwanza imetwaliwa na msomaji wa Qurani Tukufu kutoka Uturuki, akifuatiwa na qarii mwingine wa Kitabu Kitukufu cha Waislamu raia wa Misri.

Wasomaji wengine wa walioshiriki mashindano hayo wametoka katika nchi za Kuwait, Iraq, Tajikistan, Uzbekistan, Lebanon, Imarati, Sudan, Misri, Morocco, Kazakhstan, Syria, Bangladesh, na Yemen.

Kanda ya Afrika Mashariki imewakilishwa na Tanzania kwenye mashindano hayo ya kimataifa ya kusoma Qurani kwa kuzingatia kanuni za tajwidi.

Mashindano hayo ya Kimataifa ya Qurani Tukufu yameandaliwa na Baraza la Mamufti la Russia kwa ushirikiano na Jumuiya ya Waislamu Duniani.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kuandaliwa baada ya kusitishwa kwa miaka miwili, kutokana na janga la Corona lililosimamisha shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii duniani.

342/