Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

21 Novemba 2022

19:08:53
1325177

Macron: Russia inaipiga vita Ufaransa mpaka barani Afrika

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amedai kuwa Russia inaipiga vita Ufaransa mpaka barani Afrika kwa kuendesha propaganda dhidi ya nchi hiyo ya Ulaya barani humo.

Shirika la Habari Reuters limemnukuu Emmanuel Macro akisema hayo na kudai kuwa, Russia inaendelea kueneza propaganda dhidi ya Ufaransa barani Afrika kwa maslahi yake binafsi.

Ikumbukwe kuwa Ufaransa ni katika nchi za kikoloni za barani Ulaya iliyofanya ukatili na unyama mkubwa usio na kifani barani Afrika. Kila ilipoingia ilivuruga kabisa utamaduni wa Waafrika na ilisambaratisha hata lugha zao. Ingawa historia imerekodi jinai kubwa zaidi za Wafaransa huko nchini Algeria, lakini ukweli ni kwamba mkoloni huyo wa Ulaya kama ilivyo kwa wakoloni wengine wa bara hilo, wamefanya jinai nyingi zisizo na kifani dhidi ya Waafrika.

Sasa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaituhumu Russia kuwa inaeneza propaganda dhidi ya Ufaransa ili kufikia malengo yake katika nchi za Afrika kwa kusema ukweli kuhusu jinai na ukatili mkubwa wa Wafaransa barani Afrika.

Inavyoonekana ni kuwa Russia inajaribu kuwaamsha Waafrika na kuwaeleza ukweli kwamba Ufaransa inatumia vibaya uhusiano wa kikoloni, kiuchumi na kisiasa katika makoloni yake ya zamani kwa maslahi yake binafsi bila ya kujali matatizo ya makoloni hayo. Hilo limemkasirisha Macron na kumfanya adai kuwa, nchi za Afrika zinalishwa mtazamo huo na watu wengine, na eti ni mradi wa kisiasa. 

Amesema: Tunajua kuwa watu wengi wanaojitokeza kuzungumzia suala hilo wanahongwa fedha na Warusi. Ametoa madai hayo akiwa na hisia zile zile za kikoloni kwamba Waafrika hawana uwezo wa kufikiri mpaka walishwe kitu na madola ya kigeni.

342/