Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

21 Novemba 2022

19:11:09
1325181

Rais Raisi: Kushika nafasi ya kwanza katika kanda kwenye sekta ya afya ni kielelezo cha ustawi wa Iran

Rais Ebrahim Raisi amesema kushika nafasi ya kwanza katika eneo na ya kumi na tano duniani katika uga wa afya na tiba ni ishara na kielelezo cha maendeleo na ustawi wa nchi.

Rais Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo alipotembelea Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu katika kikao cha tume ya usimamizi wa vyombo vya utendaji nchini; na baada ya kusikiliza ripoti ya waziri na manaibu waziri kuhusu utendaji wa mwaka mmoja wa wizara hiyo, Seyyd Ebrahim Raisi aliongezea kwa kusema, chuki ya maadui inatokana na mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana.Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa bila shaka haikubaliki kwa maadui kuona Iran iliyo chini ya vikwazo, sio tu inazalisha asilimia 95 ya dawa zinazohitajiwa na wananchi wake, lakini pia inakuwa muuzaji dawa nje ya nchi.Katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya Novemba Mosi kubainisha hali ya sasa ya viashiria vya uzalishaji nchini, msemaji wa serikali Ali Bahadori Jahromi alisema, Iran inajitosheleza katika uzalishaji wa bidhaa 500 za matibabu.Licha ya kuwekewa vikwazo na mashinikizo ya kisiasa kimataifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kuvuka vizuizi ilivyowekewa na kupata mafankio mazuri katika nyuga za sayansi na tiba kwa kutegemea mchango muhimu wa wananchi hususan vijana wasomi wenye vipawa na wachapakazi.../

342/