Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

21 Novemba 2022

19:11:51
1325182

Iran yaamua kujibu kivitendo vikwazo vipya vya Ulaya na Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Tehran katika hatua ya awali imeazimia kujibu kwa njia tofauti, vikwazo vya hivi karibuni vya nchi tatu za Ulaya pamoja na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Itatoa majibu hayo kupitia taasisi yake ya nishati ya atomiki.

Azimio lililopendekezwa na Marekani na nchi tatu za Ulaya za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani lilipasishwa siku ya Alkhamisi kwa kura 26 za ndio, mbili za hapana na tatu za kukataa kupiga kura. Nchi za Russia na China zimepinga moja kwa moja azimio hilo.Shirika la habari la ABNA limemnukuu Nasser Kan'ani akisema jana Jumapili kwamba, Iran imeamua kuchukua hatua kadhaa kupitia taasisi yake ya nishati ya atomiki ili kujibu hatua hiyo ya nchi tatu za Ulaya pamoja na Marekani. 

Hilo ni azimio la tatu lililo dhidi ya Iran kupasishwa na Bodi ya Magavana wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA tangu yalipofikiwa mapatano ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1 ambalo baadae lilibadilika na kuwa kundi la 4+1 baada ya Marekani kujitoa. 

Wakala wa IAEA unaathiriwa moja kwa moja na misimamo ya utawala wa Kizayuni. Azimio la kwanza lilitolewa tarehe 19 Juni 2020 na la pili lilipasishwa tarehe 8 Juni 2022. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema, Tehran itaendelea kusimama kidete kulinda haki zake. Wakati wowote nchi za Magharibi zitakapoheshimu ahadi zao, Tehran nayo itaheshimu na wakati wowote zitakapochukua hatua kisiasa, Jamhuri ya Kiislamu nayo itaendelea kuonesha radimali zake kulingana na hatua hizo.

342/