Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

21 Novemba 2022

19:14:08
1325185

Idadi ya watoto waliouawa vitani nchini Yemen yapindukia 8,000

Taasisi moja ya masuala ya sheria imetangaza kuwa, idadi ya watoto waliofanywa wahanga wa vita vya muungano vamizi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen imeshapindukia elfu 8.

Shirika la habari la Mehr limeinukuu televisheni ya al Mayadeen ikiripoti habari hiyo iliyotangazwa na taasisi ya kisheria ya "Intisaf" na kuongeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa idadi hiyo ikaongezeka katika siku za usoni.

Taasisi hiyo ya masuala ya kisheria ambayo inafanya kazi katika uwanja wa haki za wanawake na watoto wa Yemen, imechapisha ripoti mpya kuhusu jinai za madola vamizi hasa Saudi Arabia na Imarati na kuongeza kuwa, muungano huo unaoongozwa na Marekani umepelekea zaidi ya watoto 8000 kuwa wahanga wa mashambulizi yao ya kinyama huko Yemen. 

Wavamizi wa Yemen wamefanya jinai kubwa mpaka ndani ya Misikiti

 

Taarifa ya taasisi hiyo imeongeza kuwa, watoto elfu nane na 116 wameuawa na kujeruhiwa nchini Yemen katika kipindi cha miaka minane tangu kuanza kwa uvamizi huo na kuongeza kuwa mashambulio ya muungano huo yamesababisha ulemavu wa raia elfu sita huku 559 kati yao wakiwa ni watoto wadogo.

Taasisi hiyo ya kisheria pia imesema, watoto milioni moja na laki nne wa Yemen wanaendelea kunyimwa haki zao za kimsingi kabisa hukuu zaidi ya watoto milioni mbili na laki tatu walio chini ya umri wa miaka mitano wakikabiliwa na utapiamlo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kila siku zaidi ya watoto 80 hufariki dunia kutokana na matumizi ya silaha zilizopigwa marufuku kimataifa. Suala hilo ni moja ya sababu za kuongezeka idadi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kiasi kwamba, kila mwaka, asilimia 39 ya watoto wa Yemen huzaliwa kabla ya wakati.

342/