Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

21 Novemba 2022

19:14:45
1325186

UN yaalani mashambulizi ya kinyama ya walowezi na wanajeshi wa Kizayuni huko al Khalil

Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi ya kinyama ya walowezi wa Kizayuni wakishirikiana na wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel huko katika mji wa al Khalil.

Wanajeshi na walowezi wa Kizayuni kila siku hushambulia maeneo mbalimbali ya Palestina kwa lengo la kufanikisha malengo yao ya kujitanua na hivyo kuwauwa shahidi, kuwajeruhi na kuwatia mbaroni raia wa Palestina. Shirika la habari la Mehr limeripoti kuwa, Tor Wennesland Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Mchakato wa Amani Magharibi mwa Asia amelaani mashambulizi na hujuma za kinyama zilizofanywa Jumamosi alasiri na walowezi wa  Kizayuni wakishirikiana na wanajeshi wa Israel katika mji wa al Khalil.  

Duru za Palestina awali zilitangaza kuhusu mashambulizi hayo ambapo ziliripoti kuwa, walowezi wa Kizayuni wakiungwa mkono pakubwa na wanajeshi wa utawala huo Jumamosi alasiri walishambulia maeneo mbalimbali katika mji wa al Khalil na hasa eneo la Babul az Zawiyah. Duru hizo ziliripoti kuwa, Wapalestina kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo, huku familia ya Badr al Batash ikifukuzwa katika makazi yao katika mji huo. 

Wanajeshi wa Kizayuni aidha waliwafyatulia risasi raia wa Kipalestia katika uvamizi wao huko Babul az Zawiyah.  Wapalestina zaidi ya laki mbili na walowezi wa kizayuni karibu ya 400 wanaishi katika mji wa al Khalil, hata hivyo katika kuendelea kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina utawala wa Kizayuni unafanya kila linalowezekana kuukalia kwa mabavu kikamilifu pia mji wa al Khalil.

342/