Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

21 Novemba 2022

19:15:33
1325187

Abdulsalam: Baadhi ya makundi ya Wayemen yanafaidika na kuendelea umwagaji damu

Mkuu wa ujumbe wa serikali ya uwokovu wa kitaifa ya Yemen katika mazungumzo ya amani ya nchi hiyo ameeleza kuwa, baadhi ya mirengo ya ndani huko Yemen yenye mfungamano na Riyadh yamegeuka na kuwa wafaidikaji katika vita huko Yemen.

Saudi Arabia huku ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi nyingine kadhaa mwezi Machi mwaka 2015 zilianzisha vita dhidi ya Yemen na kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa nchi kavu, baharini na anga. 

Muhammad Abdulsalam amesema kuwa usitishaji vita ulifikia ukomo ikiwa ni natija ya mapatano ya awali ambayo yalifikiwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa tayari umeweka mezani machaguo yake yote hata hivyo suala la kuwalipa mishahara wafanyakazi huko Yemen linaendelea kuwa takwa muhimu na kuu. 

Kuhusu nafasi ya makundi ya Wayemeni ambayo yanapigana bega kwa bega na muungano vamizi wa Saudia, Muhammad Abdulsalam amesema: mirengo hiyo ndiyo inayoichochea serikali ya Saudi Arabia kupuuza fursa za amani zinazopatikana; na hii inaonyesha namna baadhi ya makundi na mirengo ya Yemen ambayo yamekuwa yakiziunga mkono nchi vamizi yaliyojifanya  wafanyabiashara huku yakifaidika kutokana na machungu na mateso yanayowasibu wananchi wa Yemen.

342/