Main Title

source : Parstoday
Jumatano

23 Novemba 2022

17:01:09
1325670

Mgogoro wa nishati Ulaya, vyuo vikuu vya Ujerumani navyo havikusalaimika

Mgogoro wa nishati umezidi kuwa mkubwa katika nchi za Ulaya kiasi kwamba vyuo vikuu vya Ujerumani vimelazimika kuweka kwenye ajenda yake ubanaji wa matumizi ya nishati.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo leo na kuongeza kuwa, Chuo Kikuu cha Freiburg cha Ujerumani kimetoa taarifa na kusema kuwa mgogoro wa hivi sasa wa nishati umeathiri utafiti katika vyuo vikuu vyote vya nchi hiyo katika muhula wa baridi kali na ndio maana vyuo vikuu hivyo vimeweka kwenye ajenda yake, hatua kali za kubana na kupunguza mno matumizi ya nishati.

Serikali ya Ujerumani imetoa amri ya kupungua asilimia 15 ya matumizi ya nishati. Vyuo vikuu vya nchi hiyo tayari vilikuwa vimeshachukua hatua za kutekeleza amri hiyo ya serikali lakini inaonekana hazitoshi.

Mgogoro wa nishati katika nchi zote za Ulaya hasa wakati huu wa kuanza kipindi cha baridi kali, umezidi kuwa jakamoyo kwa wakazi wa bara hilo.

Jumanne ya wiki iliyopita, madereva wa vyombo vya usafiri nchini Ufaransa walishambulia vituo vya mafuta na kusababisha foleni kubwa baada ya bei ya bidhaa hiyo muhimu kupaa vibaya wakati huu wa mgogoro mkubwa wa nishati barani Ulaya.

Televisheni ya Ruptly iliripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, makumi ya madereva wa magari ya usafiri mjini Paris walivamia vituo vya mafuta kabla ya serikali ya Emanuel Macron na shirika la Total ambalo ndilo shirika kuu la mafuta nchini Ufaransa kupunguza ruzuku yake ya kufidia bei ya petroli na dizeli Jumatano iliyopita. Nchi za Ulaya zimeiwekea vikwazo Russia kwa madai ya vita vya Ukraine, lakini vikwazo hivyo vimeziweka pabaya mno nchi hizo za Magharibi. 


342/