Main Title

source : Parstoday
Jumatano

23 Novemba 2022

17:03:27
1325673

Bolsonaro alitoa wito wa kubatilishwa matokeo ya uchaguzi wa rais Brazil

Jair Bolsonaro, rais wa Brazil aliyeshindwa katika uchaguzii wa rais amewasilisha malalamiko yeke dhidi ya matokeo ya uchaguzi huo na kuiomba rasmi Tume ya Uchaguzi kufuta matokeo yake.

Bolsonaro kutoka chama cha Social Liberal Party, ambacho kimekuwa kikisimamia masuala ya Brazil tangu 2019, amesema: Wakati wa uchaguzi wa hivi majuzi wa urais, mashine za kielektroniki za kupigia kura katika vituo vingi zilikuwa na hitilafu ya programu, hivyo matokeo ya uchaguzi yanapaswa kutangazwa kuwa batili. 

Amedai kwamba iwapo Tume ya Uchaguzi ya Brazil itakubali malalamiko yake, atapata 51% ya kura sahihi na atasalia ofisini.

Jair Bolsonaro, anayejulikana kama Trump wa Brazil, alikataa kukubali kushindwa dhidi ya Lula da Silva katika hotuba yake ya kwanza baada ya uchaguzi wa rais wa hivi karibuni.

Siku ya Jumapili ya tarehe 30 Oktoba, duru ya pili ya uchaguzi wa urais ilifanyika nchini Brazili, na raia wa nchi hiyo pia walipiga kura kuwachagua magavana 12.

Katika duru ya pili ya uchaguzi huo, Luiz Inácio Lula da Silva alifanikiwa kuwa rais wa Brazil kwa mara ya pili kwa kushinda asilimia 50.8 ya kura dhidi ya asilimia 49.2 za mpinzani wake.

Rais huyo mteule wa Brazil ambaye anatarajiwa kuanza kuiongoza rasmi nchi hiyo tarehe Mosi mwaka ujao wa 2023 ameeleza bayana kwamba, ushindi wake ni kuibuka kidedea demokrasia na kwamba, Brazil inahitajia amani, umoja na mshikamano na umewadia wakati sasa wa kuwekwa kando silaha.

342/