Main Title

source : Parstoday
Jumatano

23 Novemba 2022

17:05:12
1325674

NATO yatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya mateka wa Kirussia huko Ukraine

Askari mmoja wa zamani wa jeshi la Ukraine amesema Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) limehusika katika mauaji ya mateka wa vita wa Russia huko Ukraine.

Ripoti ya Rassia Today imesema, askari wa zamani wa jeshi la Ukraine amefichua kwamba wanajeshi wa nchi hiyo waliowanyonga mateka 10 wa kivita wa Russia ni wa brigedi iliyoko katika mji wa "Lvov" ambayo inashirikiana kwa karibu na NATO.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, askari ambaye alikuwa chanzo cha habari hii aliwahi kuhudumu katika brigedi hiyo lakini alijiunga na jeshi la Russia baada ya Waukraine kumuua baba yake.

Mtandao wa Russia Today umeandika kuwa: Watu waliowekwa katika Brigedi ya 80 walifunzwa kuchukia vitu vyote vinavyohusiana na Russia muda mrefu kabla ya kuanza kwa operesheni ya kijeshi ya Russia huko Ukraine.

Ikumbukwe kwamba vikosi vya jeshi la Marekani, ikiwa ni pamoja na Jeshi la Wanamaji la nchi hiyo, vilishiriki katika kutoa mafunzo kwa brigadi hiyo.

Siku chachhe zilizopita Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitangaza kuwa wanajeshi wa Ukraine wanafanya mauaji ya kikatili dhidi ya mateka wa kivita wa Russia.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imelaani mauaji hayo ya mateka wa vita yanayofanywa na wanajeshi wa Ukraine na imezitaka jumuiya za kimataifa kulaani vikali ukatili huo na kufanya uchunguzi kamili kuhusiana na jinai hiyo.

Gazeti la Marekani la "New York Times" pia hivi karibuni lilithibitisha ukweli wa video ambayo ilisambazwa wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii ikioneshwa kunyongwa kwa wanajeshi wa Russia waliokamatwa mateka na vikosi vya Ukraine.

Video hiyo inaonesha kwamba wanajeshi hao wa Russia walipigwa risasi kwa karibu.

Awali, Tume ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilirekodi angalau uhalifu na jinai zisizopungua mbili za kivita zilizofanywa na jeshi la Ukraine katika vita vyake na Russia.

342/