Main Title

source : Parstoday
Jumatano

23 Novemba 2022

17:06:24
1325676

Iran: Madai ya Marekani na nchi za Magharibi kuhusu haki za binadamu hayana msingi wowote

Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, madai ya haki za binadamu yanayotolewa na Maraekani, nchi za Magharibi ya vibaraka wao ni chapwa na hayana msingi wowote.

Gholam Hossein Esmaili amesema hayo pembeni mwa kikao cha Baraza la Mawaziri la serikali ya Rais Ebrahim Raisi na kujibu swali la mwandishi wa shirika la habari la Iran Press akisema: Marekani, nchi za Magharibi na vibaraka wao ndio wavunjaji wakubwa wa haki za binadamu halafu zinajifanya ni viranja wa kutetea haki hizo. 

Ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran muda wote inazipa umuhimu mkubwa haki za binadamu, na inafanya hivyo kivitendo na si kwa maneno matupu tofauti ya madai ya madola ya Magharibi na vibaraka wao. 

Katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita na baada ya kutokea machafuko katika baadhi ya miji ya Iran, nchi za Magharibi ikiwemo Marekani na Canada na baadhi ya nchi za Ulaya kama Uingereza, Ujerumani na Ufaransa, kwa mara nyingine zimetumia suala la haki za binadamu kama wenzo wa kuiwekea Iran vikwazo vipya vya kiuchumi na kisiasa sambamba na kuchochoa machafuko humo nchini .

Kwa mfano nchi hizo zinajifanya ni viranja wa kutetea haki za wanawake na kutumia madai hayo kuchochea machafuko nchini Iran katika hali ambayo zinafumbia macho kikamilifu udhalilishaji mkubwa wanaofanyiwa wanawake katika jamii za nchi hizo.

Takwimu za kuaminika zinaonesha kuweko uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu hasa za wanawake na watoto wadogo katika nchi za Magharibi na katika nchi vibaraka wao, lakini madola hayo adui yanajifanya hayauoni. Marekani inaongozwa kwa biashara ya wanawake wanaotumiwa kwa ngono duniani.

342/