Main Title

source : Parstoday
Jumatano

23 Novemba 2022

17:07:00
1325677

Jeshi la Sepah lawataka wakazi wa kaskazini mwa Iraq kuwa mbali na vituo vya magaidi

Kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba jeshi hilo litaendeleza operesheni za nchi kavu dhidi ya makundi ya kigaidi yanayotaka kujitenga yaliyoko katika eneo la Kurdistan nchini Iraq hadi tishio hilo litakapotokomezwa na kupokonywa silaha magaidi hao.

Vilevile amewataka wananchi wa eneo hili kuyahama maeneo ya kandokando ya makao makuu ya magaidi hao, vituo na kambi zao.

Akizungumzia kuanza kwa duru mpya ya operesheni ya kituo cha Hamza Sayyidu Shuhadaa cha kikosi cha nchi kavu cha Sepah dhidi ya vituo na kambi za makundi ya kigaidi yanayotaka kujitenga meneo ya magharibi mwa Iran yaliyoko eneo la Kurdistan nchini Iraq, Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour amesema kuwa, katika kuendeleza operesheni za makombora na ndege zisizo na rubani za vikosi vya anchi kavu vya IRGC, duru mpya ya operesheni za makombora ya wapiganaji wa kambi ya Hamza Sayyidu al-Shuhadaa imeanza dhidi ya makao makuu na kambi za kundi la wahalifu wenye silaha na magaidi mamluki wa ubeberu wa kimataifa katika eneo la "Pardi", ndani kabisa ya eneo la Kurdistan huko Iraq. Amesema mashabulizi hayo yametoa pigo kubwa kwa magaidi hao.

Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour

Kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliongeza kuwa: Jumanne ya jana makao makuu na maeneo ya kundi la PAK ambalo limekuwa na nafasi katika kuunga mkono na kuchochea machafuko ya hivi karibuni kaskazini magharibi mwa nchi, yalilengwa na kuharibiwa kwa makombora yanayolenga shabaha kwa umakini mkubwa.

Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour amesisitiza kuwa, mashambulio ya wapiganaji wa Kiislamu dhidi ya makao makuu na vituo vya wahalifu wenye silaha na makundi ya kigaidi yanayoipiga vita Iran katika eneo la Kurdistan nchini Iraq yataendelea hadi pale tishio hilo litakapoangamizwa.

Siku ya Jumanne, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilianza duru mpya ya mashambulizi dhidi ya makundi ya kigaidi yanayotaka kujitenga baadhi ya maeneo ya Iran yenye makao yake katika eneo la Kurdistan nchini Iraq.

Mashambulizi hayo yamefanyika kwa makombora na ndege zisizo na rubani za kamikaze kwenye viunga vya mji wa Kirkuk.

342/