Main Title

source : Parstoday
Jumatano

23 Novemba 2022

17:09:41
1325682

Umoja wa Mataifa wakosoa vikali hukumu za kukatwa watu vichwa Saudi Arabia

Mmoja wa wasemaji wanaohusika na haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameelezea masikitiko yake kuhusu utekelezwaji wa hukumu za vifo kwa kukata watu vichwa nchini Saudi Arabia.

Elizabeth Trussell ameyataja mauaji yanayofanyika kwa kukata vichwa nchini Saudi Arabia kuwa ni ya kusikitisha.

Akizungumza jana Jumanne, amesema tangu Novemba 10, 2022, wanaume 17 wameuawa kwa kukatwa vichwa nchini Saudi Arabia, na hivyo idadi ya watu waliohukumiwa kifo imeongezeka hadi 144 mwaka huu.

Ripoti ya hivi karibuni inaonyesha kuwa ufalme wa Saudia unatumia vibaya kimya cha madola makubwa na jamii ya kimataifa, kuzidisha kukata watu vichwa kwa visingizio tofauti kiasi kwamba, idadi ya watu waliotekelezewa adhabu ya kifo na ukoo wa Aal Saud mwaka huu, tayari ni maradufu ya waliokatwa vichwa mwaka jana nchini humo.

Baada ya kukatwa vichwa watu wengine wawili, idadi ya watu waliotekelezewa adhabu ya kifo nchini Saudia tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022 hadi hivi sasa imefikia 138 wakati ambapo mwaka jana idadi hiyo ilikuwa ni watu 69. Tunapolinganisha mwaka huu wa 2022 na mwaka 2020, tutaona kuwa idadi ya watu waliokatwa vichwa nchini Saudia imeongezeka mara tano mwaka huu. Mwaka 2020 watu waliotekelezewa adhabu ya kifo walikuwa 27 kutokana na janga la UVIKO-19 yaani corona.

Maandamano ya kulaani sera za ufalme wa Saudia kuwakata watu vichwa

Hadi sasa makumi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Saudia wamekamatwa na vyombo vya usalama vya utawala wa Al Saud. Ingawa kukamatwa kwa wanaharakati wa Kishia na wapinzani wa utawala wa kifalme wa nchi hiyo kumekuwepo siku zote nchini Saudi Arabia, tangu mrithi wa kiti cha ufalme Mohammed bin Salman awepo tangu Juni 2017, mchakato wa kukamatwa na ukandamizaji wa Mashia na wapinzani wa utawala wa Saudi Arabia umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

342/