Main Title

source : Parstoday
Jumatano

23 Novemba 2022

17:10:11
1325683

Ajali nyingine mbaya ya barabarani yaua watu 37 nchini Nigeria

Watu wasiopungua 37 wamepoteza maisha katika ajali nyingine mbaya iliyotokea jana kaskaizni mashariki mwa Nigeria.

Polisi wa Usalama wa Barabarani wametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, ajali hiyo imehusisha mabasi mawili yaliyogongana uso kwa uso katika jimbo la kaskazini mashariki la Borno nchini Nigeria,

Utten Boyi, kamanda wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani cha serikali kuu ya Nigeria huko Borno, amewaambia waandishi wa habari kuwa, mabasi hayo yaliwaka moto baada ya kugongana kwenye barabara ya Maiduguri-Damaturu.

Boyi amesema, ajali hiyo imesababishwa na mwendo wa kasi kupita kiasi na kuongeza kwamba, mabasi hayo mawili yalikuwa yakienda katika barabara si zake. Dereva wa basi moja alishindwa kulidhibiti basi hilo na kupelekea kuacha njia yake na kugongana uso kwa uso na basi jingine.

Afisa huyo amesema wahanga hao walikuwa wamepangiwa kuzikwa pamoja katika makaburi ya umati leo Jumatano, baada ya polisi kupata agizo la mahakama la kufanya hivyo.

Ajali mbaya za barabarani zinatokea mara kwa mara nchini Nigeria. Mara nyingi husababishwa na upakiaji kupita kiasi wa abiria, hali mbaya ya barabara, uchakavu wa vyombo vya kusafiria, ulezi na kuendesha magari kwa uzembe wa kupindukia.

342/