Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

24 Novemba 2022

18:45:51
1325941

Raisi: Ustawi wa Iran unawaghadhabisha maadui

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ustawi na maendeleo yanayoshuhudiwa hapa nchini yamewakasirisha mno maadui wa taifa hili.

Rais Ebrahim Raisi amesema hayo leo Alkhamisi katika mkutano na Baraza la Utawala la Jiji Islamshahr karibu na Tehran na kuongeza kuwa, adui wa Iran anafanya kila awezalo ili kukwamisha ustawi wa taifa hili.

Rais Raisi ameeleza kuwa, "Hili ndilo linalomfanya (adui) akasirike. Anaona kunashuhudiwa ubunifu, ustawi na maendeleo kila siku katika pembe mbali mbali za nchi."

Rais wa Iran amebainisha kuwa, maadui wanatumia fedha zao katika eneo hili ili taifa hili lisistawi na liwe tegemezi kwao, lakini Jamhuri ya Kiislamu inaweza kupiga hatua bila ya kuwategemea maadui.

Sayyid Ebrahim Raisi ameeleza bayana: (Maadui) Hawataki taifa hili listawi, wanataka daima tuwategemee. Hata hivyo kutokana na jitihada za wananchi wapendwa wa Iran, nchi hii itaendelea kufuata njia ya ustawi.

Ghasia na fujo zilizojiri hivi karibuni nchini Iran kwa kisingizio cha kifo cha Mahsa Amini kwa mara nyingine tena zimetumiwa na maadui wa nchi ajinabi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama fursa ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hii na pia kuchochea pakubwa machafuko hapa nchini. 

Hata hivyo licha ya uingiliaji huo na vikwazo vya maadui, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeendelea kupiga hatua katika sekta mbalimbali ikiwemo ya teknolojia, uchumi na tiba.

342/