Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

24 Novemba 2022

18:47:07
1325943

Raisi: Machafuko ni kigingi kwa mazungumzo na ustawi wowote

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria namna serikali ilivyo na sikio la kusikia malalamiko na maoni ya upinzani na kueleza kuwa: machafuko yanazuia mazungumzo na kupatikana ustawi wa aina yoyote.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi alisema jana katika kikao na baraza la mawaziri kwamba: Machafuko ni mstari mwekundu kwa serikali na kuongeza kuwa, maandamano yanatofautiana na ghasia na fujo, na wananchi wanataraji kuwa ghasia hizo zitakabiliwa na hatua kali. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, adui ameingia kwa makusudi katika vita vya pamoja dhidi ya mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu na kulenga uhai, matumaini,  imani ya wananchi  na mtaji wa kijamii. 

Rais Raisi amebainisha kuwa, njia ya kukabiliana na ukhabithi, fitina na njama za maadui ni kujiepusha na ucheleweshaji wa aina yoyote katika kutoa huduma kwa wananchi za kuwaleta ustawi na maendeleo sambamba na  kufanya juhudi kubwa ili kutatua matatizo mbalimbali. 

Ghasia na fujo zilizojiri hivi karibuni nchini Iran kwa kisingizio cha kifo cha Mahsa Amini kwa mara nyingine tena zimetumiwa na maadui wa nchi ajinabi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama fursa ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hii na pia kuchochea pakubwa machafuko hapa nchini. 

Katika ghasia za karibuni, viongozi wa kisiasa wa Marekani na wengine kadhaa wa nchi za Ulaya, vyomvo vyao vya habari na pia vyombo vya habarizinavyorusha matangazo kwa lugha ya Kifarsi kwa kuungwa mkono kwa hali na mali na Wamagharibi walistafidi na matukio hayo ya kutisha na huku wakipiga nara na shaari za kuunga mkono haki za wananchi wa Iran hawakujizuia kuchukua hatua yoyote bali waliwauwanga mkono waziwazi waibua machafuko na kuvuruga usalama wa taifa la Iran. Wakati huo huo, mamilioni ya wananchi wa Iran walimiminika katika mitaa na maidani mbalimbali nchini wakidhihirisha uungaji mkono wao kwa mfumo na nchi yao na kutangaza kupinga vikali ghasia na machafuko hayo tajwa.   

342/