Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

24 Novemba 2022

18:47:32
1325944

Polisi ya utawala wa Kizayuni yatangaza hali ya hatari baada ya miripuko ya al Quds

Polisi ya utawala wa Kizayuni wa Israel imetangaza hali ya hatari katika ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu ikihofia uwezekano wa wana muqawama wa Palestina kuekeleza tena oparesheni dhidi ya Wazayuni.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza hali hiyo ya hatari katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ambapo vyombo vya habari jana asubuhi viliripoti kujiri miripuko miwili huko Quds inayokaliwa kwa mabavu katika kituo kikuu cha mabasi na kwenye barabara kuu ya Ramot, magharibi mwa mji wa Baytul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.Mzayuni mmoja ameangamizwa na 22 wamejeruhiwa huku hali ya watano kati yao ikiwa mahututi.

Wazayuni 2 waangamizwa katika mlipuko huko al Quds 

Televisheni ya 14 ya Israel imeripoti kuwa, polisi ya utawala huo imetangaza hali ya hatari katika ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu na imetahadharisha kuhusu kukaririwa mashambulizi ya wanamuqawama wa Palestina. 

Benny Gantz Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni, Naibu Mkuu wa Majeshi, maafisa wa kitengo cha oparesheni, itelijinsia na masuala ya kisiasa na usalama katika Wizara ya Vita pamoja na Mratibu wa Oparesheni za Polisi wamekutana katika kikao cha dharura.  

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeitaja miripuko hiyo miwili huko al Quds kuwa iliyoratibiwa na kusisitiza kuwa: oparesheni hiyo ilikuwa ya pande kadhaa kwa sababu  ni jambo lililo mbali kudhani kuwa oparesheni hiyo ilifanywa na mtu mmoja tu. 

342/