Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

25 Novemba 2022

18:01:00
1326141

Noam Chomsky: Nia ya Marekani ni kuudhofisha Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Mwanafalsafa na mwanaisimu mtajika wa Marekani Noam Chomsky amethibitisha kuwa serikali ya nchi hiyo inasaidia na kuunga mkono machafuko ndani ya Iran na akabainisha kwamba Washington inaunga mkono hatua zozote za kuudhoofisha Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hivi karibuni Marekani iliiwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutumia kisingizio cha kuunga mkono machafuko yanayojiri Iran, na katika hatua mpya ya karibuni, Wizara ya Fedha ya Marekani siku ya Jumatano iliongeza majina ya shakhsia watatu Wairan katika orodha yake ya vikwazo dhidi ya Iran.Noam Chomsky, mwanaharakati wa kisiasa, mkosoaji wa kijamii na mwanaisimu, ameeleza katika mahojiano na tovuti ya Truthout kuhusiana na machafuko ya hivi karibuni nchini Iran, kwamba: "hakuna shaka kuwa Marekani inaunga mkono hatua zozote za kuudhoofisha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambao tangu mwaka 1979 umekuwa ukihesabiwa kama adui mkuu wa Marekani".

Chomsky ameashiria pia jinsi Marekani ilivyomuunga mkono Saddam Hussein dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na akasema: "Marekani ilichukua hatua haraka sana kumuunga mkono kikamilifu rafiki yake wa wakati huo Saddam Hussein katika uvamizi wa kijinai alioanzisha dhidi ya Iran."

Kuhusu sera za mashinikizo za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, Chomsky amesema: "baada ya kumalizika vita vya Iran na Iraq, Marekani iliiwekea Iran vikwazo vikali. Rais wa Marekani wa wakati huo George Bush aliwaalika wahandisi wa nyuklia wa Iraq waende Marekani kwa ajili ya mafunzo ya kiwango cha juu ya utengenezaji silaha za nyuklia na akatuma ujumbe wa ngazi za juu nchini Iraq ili kumpa hakikisho Saddam kwamba ana uungaji mkono kamili wa Washington".Mwanafalsafa huyo mashuhuri wa Marekani amesisitiza pia kuwa vikwazo vya Ulaya na Marekani dhidi ya Iran vinawazidishia mateso wananchi wa Iran na akaongeza kwamba, Ulaya inauchukulia ushirikiano wake wa kibiashara na Iran kuwa ni fursa ya uwekezaji, biashara na uchimbaji maliasili, lakini sera za Marekani za kuikandamiza Iran zimeziba fursa zote hizo kwa nchi za Ulaya.../


342/