Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

25 Novemba 2022

18:02:12
1326143

Mgomo wa wahadhiri 70,000 katika vyuo 150 Uingereza kuathiri wanafunzi zaidi milioni 2.5

Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini Uingereza wameanzisha mgomo wa nchi nzima kulalamikia mishahara yao na mazingira ya kazi.

Zaidi ya wahadhiri, watafiti na wakutubi elfu sabini wa vyuo vikuu 150 vya Uingereza wamefanya mgomo kwa siku tatu ulioanza jana Alhamisi na kuendelea leo Ijumaa kabla ya kurudiwa tena siku ya Jumatano ijayo, hatua ambayo itaathiri na kukwamisha masomo ya wanachuo zaidi ya milioni mbili na nusu wa vyuo vikuu vya nchi hiyo.Wasimamizi wa vyuo vikuu, wasafishaji, walinzi wa usalama na wapishi ambao ni wanachama wa Chama cha Wahadhiri wa vyuo vikuu vya Uingereza (UCU) katika vyuo vikuu 19, nao pia wametangaza kujiunga na mgomo huo.Mgomo huo wahadhiri wa vyuo vikuu umetajwa kuwa mkubwa zaidi kuwahi kufanywa katika historia ya Uingereza katika taasisi za elimu ya juu.Madai ya UCU ni pamoja na nyongeza ya mishahara kwa kuzingatia hali mbaya ya gharama za maisha iliyopo hivi sasa mbali na nyongeza ya asilima tatu iliyotolewa mwaka huu, na vilevile kufutwa mikataba inayohatarisha usalama wa ajira zao.

Kwa upande wa pensheni, Chama cha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya Uingereza kinawataka waajiri wabadili punguzo lililowekwa mwaka huu ambalo kinadai litapelekea wanachama wake wengi kupoteza takriban 35% ya mapato yake ya baada ya kustaafu.

UCU imelalamika kuwa, kiwango cha pensheni kinacholipwa kinawafanya wahadhiri wastaafu wakidhi kwa tabu gharama zao za maisha na kwamba kuna ulazima pia wa kuhakikishwa uthabiti wa kiuchumi unapatikana katika nchi hiyo.Wasiwasi mwingine wa wahadhiri wa vyo vikuu vya Uingereza mbali na mishahara na mazingira ya kazi ni pensheni ya kustaafu.Uchumi wa Uingereza uko katika hali mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha nusu karne sasa kutokana na migogoro kadhaa ya mtawalia.Ingawa nchi zote za Ulaya zimekumbwa na mtikisiko wa kiuchumi huku mfumuko wa bei ukiongezeka kwa kasi, lakini takwimu na tafiti zinaonyesha kuwa Uingereza iko katika hali mbaya zaidi katika kila uga ikilinganishwa na nchi zote wanachama wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD).../


342/