Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

25 Novemba 2022

18:03:21
1326145

Amir-Abdolahian: Ujerumani kwa miaka mingi inavunja haki za binadamu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu madai yasiyo na msingi ya waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani aliyoyatoa katika kikao maalumu cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa mataifa na kusema kwamba, kwa miaka mingi Ujerumani inavunja haki za binadamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Hossein Amir-Abdollahian ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, utawala wa kibeberu wa Berlin ndio uliompa silaha za kemikali Saddam ambaye alizitumia silaha hizo kuulia wananchi wa Iran. Kwa miaka mingi Ujerumani inashiriki katika vikwazo vya kidhulma na visivyo na chembe ya utu dhidi ya wananchi wa Iran. Leo lakini inajifanya kuwapenda sana wananchi wa Iran.

Jana Alkhamisi, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio dhidi ya Iran kwa madai ya eti uvunjaji wa haki za binadamu.

Jana hiyo hiyo, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, alidai katika hotuba aliyoitoa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi kwamba anaungana na nchi nyingine za Magharibi kuelezea wasiwasi wake kuhusu haki za binadamu nchini Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu madai hayo yasiyo na msingi akisema, Ujerumani inatumia vibaya suala la haki za binadamu ili iweze kushiriki zaidi katika hatua zilizo dhidi ya wananchi wa Iran. Yote hayo yanafanyika kwa madai ya uongo wa eti kuwa pamoja na wananchi wa Iran.

342/