Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

25 Novemba 2022

18:03:51
1326146

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaonuya kuhusiana na jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

Katibu Mkuuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ameonya kuhusiana na jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina na kueleza kwamba, zitakuwa na matokeo mabaya zaidi.

Ahmad Abul-Gheit, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa, ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina uko kwa namna ambayo unatishia hali ya mambo kulipuka katika ardhi za Palestina na hivyo kuwa na matokeo mabaya zaidi.

Akiizungumza leo Abdul-Gheit ameashiria hali ya mambo duniani na kueleza kuwa, migogoro mipya inayoibuka katika maeneo tofauti ya ulimwengu haipaswi kuwa sababu ya kufunikwa na kusahalika migogoro ya Asia Magharibi ukiwemo mgogoro mkubwa zaidi katika eneo hili yaani kadhia ya Palestina. 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ameongeza kuwa, wananchi wa Palestina wanataabika kwa masaibu ambayo chimbuko lake ni Israel na kwamba, yanayofanywa na utawala huo dhidi ya Wapalestina hayana utambulisho mwingine mwingine ghairi ya  ubaguzi wa rangi wa apartheid.

Kwa zaidi ya miaka 70 sasa ambapo haki za Wapalestina zimekuwa zikiporwa  waziwazi na utawala ghasibu wa Israel unaoungwa mkono na madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani. Katika kipindi hiki utawala vamizi wa Israel umetenda jinai za kutisha dhidi ya Wapalestina huku Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama zikiwa watazamaji .

342/