Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

25 Novemba 2022

18:04:50
1326148

Utawala dhalimu wa Israel umebomoa zaidi ya skuli 50 za Wapalestina katika mwaka huu

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Umoja wa Mataifa, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umebomoa zaidi ya skuli 50 za Wapalestina katika mwaka huu wa 2022.

Ili kufikia malengo yao ya kujipanua, Wazayuni huvamia kila siku maeneo tofauti ya Palestina na kuwaua shahidi, kuwajeruhi au kuwatia nguvuni Wapalestina wasio na hatia.Kuhusiana na suala hilo, na kwa mujibu wa ripoti ya kanali ya televisheni ya Al Jazeera, askari wa utawala wa Kizayuni wamebomoa skuli moja katika miinuko ya kusini ya mji wa al Khalil.Skuli hiyo ni moja ya skuli zisizopungua hamsini zilizobomolewa na askari katili wa utawala haramu wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.Utawala wa Kizayuni unachukua hatua ya kuzibomoa skuli za Wapalestina kwa madai kwamba skuli hizo zimejengwa bila ya kibali.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, utawala dhalimu wa Israel umezibomoa pia zaidi ya nyumba 730 za Wapalestina katika mwaka huu wa 2022.

Kwa zaidi ya miaka 70 sasa, haki za wananchi madhulumu wa Palestina zinaendelea kukanyagwa na kupokwa na utawala ghasibu wa Kizayuni. Kwa muda wa miaka yote hiyo utawala huo haramu umetenda jinai za kinyama kupindukia dhidi ya Wapalestina.../

 

342/