Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

26 Novemba 2022

18:33:31
1326423

Umoja wa Mataifa: Video za kunyongwa wanajeshi wa Russia huko Ukraine ni za kweli

Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kwamba kuna uwezekani mkubwa kwamba video za kunyongwa wanajeshi wa Russia waliotekwa nyara huko Ukraine ni za kweli.

Kulingana na shirika la habari la IRNA, Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, amesema katika taarifa yake kwamba matokeo ya uhakiki wa video hizo yanathibitisha kwamba uchunguzi huru na sahihi wa kisheria unapaswa kufanywa ili kujua ni nini hasa kilichotokea.

Turk amesisitiza kuwa: Mashtaka yote kuhusu mauaji ya kiholela yanapaswa kuchunguzwa kikamilifu na kwa njia huru, isiyo na upendeleo, ya uwazi, ya haraka na yenye ufanisi.

Gazeti la Marekani la "New York Times" hivi karibuni lilithibitisha ukweli wa video ambayo ilisambazwa wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii ikioneshwa kunyongwa kwa wanajeshi wa Russia waliokamatwa mateka na vikosi vya jesi la Ukraine.

Video hiyo inaonesha kwamba wanajeshi hao wa Russia walipigwa risasi kwa karibu.

Awali, Tume ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilirekodi angalau uhalifu na jinai zisizopungua mbili za kivita zilizofanywa na jeshi la Ukraine katika vita vyake na Russia.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imelaani mauaji hayo ya mateka wa vita yanayofanywa na wanajeshi wa Ukraine na imezitaka jumuiya za kimataifa kulaani vikali ukatili huo na kufanya uchunguzi kamili kuhusiana na jinai hiyo.

Ripoti ya Rassia Today imesema, askari wa zamani wa jeshi la Ukraine amefichua kwamba wanajeshi wa nchi hiyo waliowanyonga mateka 10 wa kivita wa Russia ni wa brigedi iliyoko katika mji wa "Lvov" ambayo inashirikiana kwa karibu na NATO.


342/