Main Title

source : Parstoday
Jumapili

27 Novemba 2022

16:45:03
1326729

Jeshi la Somalia lachukua udhibiti wa mji wa kimkakati wa El Dhere kutoka Al Shabab

Serikali ya Somalia siku ya Jumamosi ilitangaza kuwa jeshi la nchi hiyo limechukua tena udhibiti wa mji wa kimkakati wa El Dhere kutoka kwa kundi la kigaidi la al-Shabaab.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Abdirahman Yusuf al-Adala, naibu waziri wa habari, alisema kuwa zaidi ya magaidi 100 wa al-Shabaab, wakiwemo makamanda wao 12, waliuawa katika eneo la Shabelle ya Kati katika operesheni ya kijeshi inayoungwa mkono na wanamgambo wa ndani na usalama wa kimataifa. 

Alisema operesheni hiyo ilifuatiwa na operesheni sawia ya kijeshi katika kijiji cha Bulo-Madino kusini magharibi mwa mkoa wa Lower Shabelle ambapo zaidi ya magaidi 60 wa al-Shabaab waliuawa.

Siku ya Ijumaa, jeshi lilisema lilizuia shambulio la al-Shabaab kwenye kambi ya kijeshi katika eneo la kati la Galgadud.

Somalia imekuwa ikikumbwa na ukosefu wa usalama kwa miaka mingi, huku magaidi wa al-Shabaab wakiwa  mojawapo ya vitisho vikuu.

Tangu 2007, al-Shabaab wameendesha kampeni mbaya dhidi ya serikali ya Somalia na vikosi vya kimataifa, na kupelekea maelfu ya watu kupoteza maisha.

Umoja wa Mataifa pia umeonya juu ya kuongezeka ukosefu wa utulivu nchini humo, huku ripoti zake za mara kwa mara kuhusu Somalia mwaka huu zikielezea mashambulizi ya al-Shabaab na makundi yanayounga mkono Daesh au ISIS.

Al Shabab ni kundi la kigaidi linalobeba silaha lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida ambalo limehusika katika hujuma na mashambulizi mengi ya kigaidi yaliyouwa mamia ya watu katika nchi mbalimbali barani Afrika.  

342/