Main Title

source : Parstoday
Jumapili

27 Novemba 2022

16:45:56
1326730

Economist: Idadi ya vifo katika majira ya baridi kali Ulaya ni zaidi ya vita vya Ukraine

Kwa mujibu wa uchambuzi mpya uliofanywa karibuni, idadi ya watu ambao watapoteza maisha katika msimu wa baridi kali barani Ulaya mwaka huu kutokana na uhaba wa nishati itakuwa zaidi ya wale waliouawa katika vita huko Ukraine.

Bei ya nishati ya gesi na umeme kwa ajili ya matumizi ya nyumbani huko Ulaya imeongezeka pakubwa ikiwa ni natija ya vikwazo vikubwa vya nchi za Magharibi dhidi ya Russia kwa kisingizio cha vita huko Ukraine. Kabla ya vita, Russia ilikuwa ikizidhaminia nchi za Ulaya asilimia 40 hadi 50 ya gesi asilia.  

Jarida la Economist limetoa hitimisho kuwa, kuna uwezekano wa kutokea vifo 147,000 katika msimu wa baridi kali huko Ulaya kwa kuzingatia gharama za sasa za kupanda kwa bei ya nishati. Aidha iwapo baridi itaongezeka na kuwa kali zaidi idadi ya vifo itafikia 185,000 huko Ulaya. 

Takwimu za jarida la Economist zinajumuisha nchi zote za Umoja wa Ulaya, zikiwemo Uingereza, Norway na Uswisi. Aidha imebainika kuwa, Estonia na Finland zitaathiriwa na vifo vingi vya watu katika msimu wa baridi kali mwaka huu.  

Wakati huo huo,  Uingereza na Ufaransa zitakuwa na hali nzuri kutokana na kutangaza ukomo wa bei ya nishati;na huko Austria pia vifo ambavyo vingesababishwa wakati wa msimu wa baridi kali vinatazamiwa kupungua kutokana na nchi hiyo kuwa na bei ya wastani ya nishati.

342/