Main Title

source : Parstoday
Jumapili

27 Novemba 2022

16:48:47
1326733

Rais Raisi: Pwani ya Makran ni eneo la kistratijia kwa Iran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria umuhimu wa Pwani ya Makran katika uchumi wa baharini na kusema: "Eneo hili linaweza kuwa eneo la kistratijia katika nchi".

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo Jumapili alipohutubia halaiki kubwa ya wananchi katika Bandari ya Jask na kuongeza kuwa: "Pwani ya Makran inaweza kuwa kituo cha kiuchumi, kibiashara na kiviwanda nchini Iran."

Raisi amesema kuna uwezo mkubwa katika Pwani ya Makran na ambao unaweza kuibadilisha pwani hii kuwa eneo muhimu sana na la kimkakati kwa mtazamo wa kibiashara, kiuchumi, kitalii na kiviwanda nchini Iran.

Punde baada ya kuwasili Hormozgan mapema leo asubuhi, Rais ametembelea eneo kubwa la Jask na pwani yote ya Makran.

Akiwa katika eneo hilo Raisi pia ametembelea kituo cha Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo amekagua gwaride maalmu ya meli za kivita na nyambizi. Aidha amewasiliana kwa njia ya video na manowari za Iran zinazolinda doria katika Bahari ya Sham na Bahari ya Pasifiki.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Makran ni pwani iliyoko kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  na ina umuhimu mkubwa wa kistratijia.

Karibu thuluthi moja ya mipaka ya Iran ni ya baharini ambapo kilimota 800 ya mipaka hiyo iko katika pwani ya kaskazini huku kilimota 2000 zikiwa katika pwani ya Ghuba ya Uajemi na Pwani ya Makran kusini mwa Iran.

Pwani ya Makran inaunganisha Iran na bahari ya kimataifa na iwapo uwezo wa eneo hilo utatumika ipasavyo basi linaweza kuwa kitovu kikubwa cha ustawi wa kiuchumi.  

342/