Main Title

source : Parstoday
Jumapili

27 Novemba 2022

16:49:32
1326734

Kamanda wa IRGC: Tutabadilisha fitina ya karibuni kuwa kaburi kwa Wamarekani na Waisraeli

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa leo Marekani, Uingereza, Israel na Saudia zimejitokeza katika medani lakini kwa yakini fitina hii kubwa walioanzisha, na vita hivi vya dunia walivyoibua vitabadilika na kuwa kaburi la maadui wakiwemo Wamarekani, Waisraeli na waitifaki wao.

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) leo akizingumza mbele ya maelefu ya wananchi mjini Zahedan katika mkoa wa Sistan na Baluchestan amesema: "Iwapo tunataka kuwa na taswira ya usharifu, heshima na uhuru wa mwanadamu basi taswira hiyo iko katika mkoa wa Sistan na Baluchestan."

Kamanda Mkuu wa IRGC ameongeza kuwa: "Wakati Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni wanapouawa shahidi pamoja wakiwatetea wananchi wa taifa hili, na dani ya wanadamu ambao ni waumini zaidi inapomwagwa katika tukio la kigaidi, basi matukio yanakuwa ni chumbuko la umoja usioweza kuvunjika."

Meja Jenerali Salami ameendelea kuwa: "Wakati magaidi wakufurishaji walio chini ya usimamizi wa Marekani, Utawala wa Kizayuni na Ulaya walipovamia Syria, Lebanon, Iraq na Yemen, ni Mabasiji waliongia katika medani huku wakiacha nyumba zao na kuingia katika kitovu cha maadui na hatimaye wakafanikiwa kuyaokoa mataifa yaliyokuwa yametekwa nyara na maajinabi."

Meja Jenerali Salami ameongeza kuwa maadui wana ndoto nyingi za alinacha na hawajui kuwa Iran na Mapinduzi yake ya Kiislamu ni imara.

342/