Main Title

source : Parstoday
Jumapili

27 Novemba 2022

16:51:24
1326736

Waziri Mkuu wa Iraq kufanya ziara Tehran Jumatatu

Vyombo vya habari vya Iraq vimetangaza kuwa Mohammed Shia al Sudani Waziri Mkuu wa Iraq kesho Jumatatu atafanya ziara hapa mjini Tehran.

Mohammad-Kazem Ale-Sadegh Balozi wa Iran huko Iraq jana Jumamosi alikutana na Mohammed Shia al Sudani na kumtaarifu kuhusu mwaliko wa Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kuitembelea Iran. 

Hii ni ziara ya tatu nje ya nchi kufanywa na al Sudani tangu awe Waziri Mkuu wa Iraq, baada ya kuzitembelea Jordan na Kuwait. Iraq ni miongoni mwa nchi za eneo la Asia Magharibi iliyo na mafungamano makubwa sana ya kiutamaduni na kidini na Iran.  

Kati ya nukta muhimu zinazoshuhudiwa katika uhusiano wa Iran na Iraq ni kule kuwepo kwa mpaka mrefu zaidi kati ya nchi jirani wenye masafa karibu kilomita 1258 kwa upande wa nchi kavu na kwa upande wa baharini ukiwa na urefu wa kilomita 351, kuwepo mahusiano ya kijamii, kihistoria, kilugha, maingiliano ya kidini, vitisho na maslahi ya pamoja ya kiusalama na kiuchumi. 

342/