Main Title

source : Parstoday
Jumanne

10 Januari 2023

15:37:06
1337451

Amir- Abdollahian aunga mkono uwepo wa wanawake wanadiplomasia katika nyadhifa za uongozi

Hossein Amir- Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amebainisha wazi mtazamo wa chombo hicho cha diplomasia cha nchi kuhusu wanawake kuhudumu katika wizara hiyo, na kusisitiza mtazamo wa wizara hiyo katika kusaidia na kuwezesha uwepo wa ufanisi zaidi wa wanadiplomasia wa kike katika nyadhifa za uongozi ndani na nje ya nchi. • Feedback

Hafla maalumu kwa mnasaba wa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Bibi Fatima az- Zahra (SA) binti wa Mtume Muhammad (SAW) na maadhimisho ya Siku ya Mwanamke ilifanyika jana Jumatatu kwa kuhudhuriwa na Hossein Amir-Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje, wakurugenzi, wataalamu na wafanyakazi wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran.  

Katika hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekutaja kutengwa siku maalumu kwa jina la "Siku ya Mwanamke" hapa nchini; siku aliyozaliwa Mtukufu Bibi Fatima az-Zahra, Siddiqat al Kubra (SA) kuwa ni jambo la thamani na la kujivunia. 

Amir- Abdollahian ametaja madhumuni ya harakati ya wanawake wa Kiirani katika njia ya mafunzo ya mtukufu huyo wa duniani na Akhera kuwa ni harakati iliyostawi mkabala wa wanawake wa Iran ya Kiislamu.    

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameelezea wazi mtazamo wa chombo cha diplomasia cha nchi hii kuhusu wanawake wa wizara hiyo na kuitaja nafasi ya wanawake wanadiplomasia katika kuarifisha uwezo, vipawa na nafasi ya mwanamke wa Kiirani katika nyuga za kimataifa kuwa yenye umuhimu maalumu. Hossein Amir-Abdollahian amesisitiza pia kuhusu hatua za Wizara ya Mambo ya Nje za kuwaunga mkono na kusaidia ushiriki vyema na wenye taathira wa wanawake wanadiplomasia katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani na nje ya nchi. 

342/