Main Title

source : Parstoday
Jumanne

10 Januari 2023

15:38:13
1337453

Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu; lengo la fujo lilikuwa ni kusambaratisha nguvu za nchi na si kuondoa udhaifu

Machafuko yaliyozuka hivi karibuni nchini Iran kwa kisingizo cha kifo cha Mahsa Amini, yalitumiwa na maadui ajinabi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama fursa ya kuingilia masuala ya ndani ya taifa hili na wakati huo huo kuchochea zaidi moto wa fujo na vurugu zilizokuwa zimeanzisha na watu wachache waliohadaiwa.

Ukweli wa mambo ni kuwa, katika fujo na ghasia hizo ambazo zilibadilika na kuwa ugaidi, watawala wa kisiasa wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya na vyombo vyao vya habari na halikadhalika vyombo vya habari vinavyopinga Mapinduzi ya Kiislamu vya lugha ya Kifarsi ambavyo vinaungwa mkono na madola ya magharibi na watifaki wao, vilianza kudai kuunga mkono haki za taifa la Iran na kufanya kila lililowezekana kuunga mkono ghasia na kuvuruga usalama wa taifa la Iran.

Hivyo bassi maadui wa Iran walituumia vibaya tukio chungu la kifo cha Mahsa Amini kwa ajili ya kufikia malengo yao. Madola ya Magharibi hususan Marekani ilifanya kila iwezalo na kutoa ahadi kama za kuondoa vikwazo vya mitandao ya kijamii na mawasiliano ya intaneti na kwa muktadha huo ikawa imeweka wazi msimamo wake ambao ni kuwa pamoja na wafanyafujo. Hata hivyo utawala wa Marekani ulishindwa kufikia malengo yake baada ya ndoto zake hizo kuota mbawa. Hatua iliyofuata ikawa ni kambi ya Magharibi yaani Marekani na Umoja wa Ulaya kuwa pamoja na Canada na Australia katika kuziwekea vikwazo vya hatua kwa hatua asasi na baadhi ya maafisa wa serikali nchini Iran kwa kisingizio kwamba, walisimama na kukabiliana na waandamanaji ambao kimsingi ni wafanyafujo ambao walikuwa wakiharibu mali za watu na za umma.

Vikwazo hivi ambavyo viliwekwa kwa kisingizio cha kuwaunga mkono wananchi wa Iran sio tu kwamba, ni uingiliaji wa wazi wa masuala ya ndani ya nchi yenye mamlaka ya kujitawala hatua ambayo inakinzana dhahir shahir na sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa, bali ni ishara nyingine ya wazi ya utendaji usio na nia njema na wa kinafiki wa Wamagharibi mkabala na wananchi wa Iran.

Suala ambalo Wamagharibi wamelizungumza na kulipigia upatu mara chungu nzima iwe ni viongozi au vyombo vyao vya habari ni kuwa, wanacholalamikia wananchi wa Iran ni nakisi na mapungufu na vilevile udhaifu uliopo katika nchi yao. Hii ni katika hali ambayo kinyume na madai yao hayo, sababu kuu ya madola hayo kuwaunga mkono wananchi wachache waliohadaiwa hapa nchini na kujificha nyuma ya tukio la kifo cha Mahsa Amini ni hofu na woga mkubwa walionao wa kupiga hatua na ustawi wa maendeleo Iran katika nyuga mbambali iwe ni medani za maendeleo ya teknolojia ya nyuklia, uwezo wa kijeshi hususan makombora na ndege zisizo na rubani (droni). Hivyo madola hayo yalikuwa yakiota ndoto za alinacha kwa kudhani kwamba, kwa kuwaunga mkono wafanyafujo wataweza kuirejesha nyuma Iran na kusimamisha kasi yake ya ustawi na maendeleo.

Katika kipindi cha miongo minne baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, taifa hili limepiga hatua kubwa na za kushangaza katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii, kijeshi, kiviwanda, kilimo na teknolojia, maendeleo ambayo yamewafanya hata maadui wa taifa hili wasiwe na budi isipokuwa kukiri wazi na bayana. Katika kipindi hiki Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kupiga hatua kubwa na kufikia kiwango cha kujitosheleza katika mambo mengi na kuondokana kabisa na hali ya utegemezi wa kigeni.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake alipokutana jana Jumatatu hapa mjini Tehran na wakazi wa mji wa Qum kwa mnasaba wa maadhimisho ya kukumbuka mapambano ya kihistoria ya watu wa mji huo mnamo tarehe 19 mwezi Dei mwaka 1356 Hijria Shamsiya iliyosadifiana na Januari 9 mwaka 1978, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliashiria machafuko ya hivi karibuni  nchini Iran na kusema: Baadhi ya watu walitaka kuonyesha na maajinaabi walikuwa wakionyesha katika propaganda zao kwamba, hii kwamba, baadhi ya watu wanajitokeza barabarani, wanapiga mayowe, kutoa matusi na wakati mwingine wanavunja vioo na kuchoma moto vifaa vya kuwekea taka na hatua nyingine kwamba, haya yanatokana na udhaifu wa nchi, udhaifu wa uongozi, uchumi na kadhalika, lakini ukweli wa mambo hauko hivyo. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Watu ambao walijitokeza na kujihusisha na fujo na machafuko lengo lao halikuwa kuondoa udhaifu na mapungufu bali lilikuwa ni kusambaratisha nukta ambazo zinaipa nguvu nchi hii. Bila shaka hii ilikuwa ni khiyyana na usaliti na vyombo husika vinaamiliana na wahusika kwa mamlaka kamili na kwa uadilifu, na bila shaka vinapaswa kufanya hivyo.

342/