Main Title

source : Parstoday
Jumatano

11 Januari 2023

16:56:11
1337776

UN: Afrika na Asia Kusini zinaongoza kwa vifo vya watoto

Umoja wa Mataifa umesema eneo la chini ya jangwa la Sahara barani Afrika na kusini mwa bara Asia ndiyo maeneo yanayosajili vifo vingi zaidi vya watoto kutokana na ukosefu wa vituo na taasisi za afya.

Ripoti iliyochapishwa jana Jumanne katika tovuti ya Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) inaonesha kuwa, watoto milioni 5 walifariki dunia mwaka 2021 kabla ya kufikisha miaka mitano, huku wengine wapatao milioni 2.1 wakiwemo vijana waliokuwa na umri wa kati ya miaka 5-27 wakiaga dunia katika maeneo hayo tajwa mwaka huo.

Utafiti wa makadirio ya vifo vya watoto uliofanywa na taasisi kadhaa za Umoja wa Mataifa umeonyesha kuwa, asilimia 77 ya vifo vya watoto milioni 1.9 waliozaliwa kama tayari wamepoteza maisha au wakati wa kuzaliwa iliripotiwa katika eneo la chini ya jangwa la Sahara barani Afrika na kusini mwa bara Asia 2021.

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo, asilimia 40 vifo hivyo vya watoto kabla au wakati wa kuzaliwa vilitokea wakati wa uchungu wa uzazi, na aghalabu yake vingeweza kuzuilika iwapo wazazi wangelipokea huduma faafu katika taasisi bora za afya.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa, watoto na vijana milioni 59 zaidi huenda wataaga dunia iwapo huduma za afya haziboroshwa katika maeneo hayo kufikia mwaka 2023, na wengine milioni 16  wataaga dunia kabla au wakati wa kuzaliwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti hiyo, kwa ujumla vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua duniani kwa asilimia 50 tangu mwanzoni mwa karne hii, huku vile vya kabla au wakati wa kuzaliwa vikipungua kwa asilimia 36.

342/