Main Title

source : Parstoday
Jumatano

11 Januari 2023

16:56:40
1337777

Russia: Vikwazo vya Magharibi vimeshadidisha hali mbaya ya kibinadamu Syria

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema Wamagharibi wanabeba dhima ya kushtadi hali mbaya ya kibinadamu nchini Syria kutokana na vikwazo vyao vya upande mmoja.

Vasily Nebenzya amesema hayo kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa, "Jumbe za Magharibi zimeakisi kwa kina juhudi zao za kuwafikishia Wasyria misaada ya kibinadamu, lakini zimefumbia macho maudhui wasiopenda kuigusia; ambayo ni vikwazo vyao vya kijinai na vya upande mmoja ambavyo vinawaumiza wananchi wa kawaida wa Syria."

Nebenzya amebainisha hayo baada ya Baraza la Usalama kupasisha azimio linalohusu mpango wa kuwafikishia Wasyria misaada ya kibinadamu hadi ambao umeongezewa muda wake hadi Julai 10 mwaka huu.

Mwanadiplomasia huyo wa Russia ameongeza kuwa, kupuuza mateso wanayopata Wasyria kutokana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya kuna madhara na maafa makubwa kwa maisha ya kila siku ya raia na hakuwaruhusu kupata huduma muhimu na za dharura kama gesi na umeme, hasa wakati huu wa msimu wa baridi kali.

Nebenzya amesisitiza kuwa, Magharibi inashadidisha kwa makusudi mgogoro wa kibinadamu nchini Syria, kwa lengo la kujaribu kuifanya ya kawaida hali ya nchi hiyo, na wakati huohuo kukosoa hatua zinazopigwa na serikali halali ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Syria imesisitiza mara kadhaa kwamba, kimya kinachozidi kuonyeshwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na sera za kichokozi za Wamagharibi wakiongozwa na Marekani na ukiukaji wa misingi ya sheria za kimataifa ni jambo lisilokubalika.


342/