Main Title

source : Parstoday
Jumatano

11 Januari 2023

16:59:52
1337784

Marekani yaongeza ulinzi kwa viongozi wa serikali ya Trump waliomuua Kamanda Soleimani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kila mwezi inatumia zaidi ya dola milioni mbili kuwalinda saa 24 Mike Pompeo na Brian Hook, viongozi wa serikali ya Donald Trump waliohusika katika mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Marekani la Associated Press, serikali ya Joe Biden kwa mara nyingine imeongeza muda wa mpango wa kuwalinda Mike Pompeo, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani wa wakati wa serikali ya Donald Trump na Brian Hook, ambao wote wawili walikuwa washauri wakuu wa Trump, kwa hofu ya kulipiziwa kisasi na Iran.

Wiki iliyopita, wizara ya mambo ya nje ya Marekani iliwasilisha taarifa tofauti kwa Baraza la Congess na kusema kuwa, tishio la usalama kwa Pompeo na Brian Hook bado ni kubwa. Hook alikuwa mwakilishi maalumu wa serikali ya Trump kuhusu Iran.

Brian Hook na Pompeo ndio waliokuwa viranja wa kampeni za kuiwekea Iran vikwazo vya hali ya juu baada ya Marekani kujitoa kijeuri kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Iran inawahesabu Hook na Pompeo kuwa wahusika wa kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi SEPAH na mara kwa mara viongozi wa Iran wanasisitiza kuwa, kisasi cha mauaji hayo bado hakijachukuliwa. 

Tangu wakati huo hadi hivi sasa, wizara ya mambo ya nje ya Marekani kila mwezi huwa inatumia zaidi ya dola milioni mbili za kuwapa ulinzi wa saa 24 Hook na Pompeo.

342/