Main Title

source : Parstoday
Jumatano

11 Januari 2023

17:00:20
1337785

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC yataka Mzayuni Ben-Gvir awekewe vikwazo

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeitisha kikao cha dharura cha kuchunguza kuvunjiwa heshima Msikiti wa Al-Aqsa na Wazayuni wenye itikadi kali. Kikao hicho kimefanyika mjini Jeddah Saudi Arabia na kusisitiza kuwekewa vikwazo waziri wa usalama wa ndani wa utawala wa Kizayuni.

Itamar Ben-Gvir, waziri wa usalama wa ndani wa utawala wa Kizayuni wa Israel hivi karibuni aliuvamia Msikiti wa al Aqsa, ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu akilindwa kikamilifu na jeshi la utawala wa Kizayuni Jumanne ya wiki iliyopita.

Hatua ya Ben-Gvir imeukasirisha mno Ulimwengu wa Kiislamu na hasa Wapalestina na Waarabu na makundi ya muqawama ya Palestina.

Nchi za Kiarabu zikiwemo Qatar, Jordan, Imarati, Saudi Arabia, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki zimelaani. Kwa upande wake, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa zaidi ya miongo minne sasa iko mstari wa mbele kupigania ukombozi wa Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sputnik, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imelaani uvamizi wa shambulizi wa hivi karibuni la "Itamar Ben-Gvir" dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa na kulivunjiwa heshima eneo hilo takatifu.

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu pia imetahadharisha kuhusu madhara ya kuendelea kuvunjiwa heshima Msikiti wa Al-Aqswa na kutangaza kuwa, kitendo hicho ni uchochezi mkubwa uliotonesha hisia za Waislamu kote duniani na ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu aidha imeutaka utawala wa Kizayuni kuwajibika na kubeba lawama ya matukio yanayotokea kufuatia kitendo hicho cha uchochezi na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka za kuzuia, kulaani na kukomesha kushadidi chokochoko za Wazayuni.

342/