Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

13 Januari 2023

15:13:54
1338088

Uturuki: Zaidi ya tani milioni tano za nafaka zimepelekwa kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu ambaye yuko ziarani barani Afrika amesema, kufuatia makubaliano ya utumaji nafaka za Ukraine, yanayojulikana kama "Makubaliano ya Istanbul", zaidi ya tani milioni tano za nafaka zimefikishwa katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Çavuşoğlu ameyasema hayo Kigali, mji mkuu wa Rwanda jana usiku katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na waziri mwenzake wa Rwanda Vincent Biruta.Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki ameongezea kwa kusema,"makubaliano ya nafaka yamewezesha pia kuuzwa tani milioni 17 za nafaka, ambazo zimesafirishwa kuelekea nchi tofauti kupitia Bahari Nyeusi."Aidha amesema, zaidi ya 60% ya nafaka za Ukraine zimesafirishwa kuuzwa nje kwa nchi za kipato cha chini na cha kati.Siku mbili kabla ya hapo, Çavuşoğlu, alisisitiza katika mkutano mwingine aliofanya na waziri mwenzake wa Afrika Kusini Naledi Pandor huko mjini Pretoria juu ya udharura wa kupelekwa nafaka zaidi na mbolea barani Afrika, na katika nchi zinazoendelea na zenye ustawi mdogo.Mevlut Cavusoglu

Russia na Ukraine ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa nafaka duniani. Kuanza kwa vita huko Ukraine na vikwazo vya Magharibi dhidi ya Russia vimesababisha kupanda bei ya nafaka ulimwenguni.

Baada ya kusitisha usafirshaji kwa takriban miezi sita kutokana na vita vya Ukraine, bandari tatu za Bahari Nyeusi za Ukraine zilifunguliwa mwishoni mwa Julai chini ya makubaliano kati ya Moscow na Kyiv yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki.Makubaliano ya awali juu ya usafirishaji wa nafaka za Ukraine yalikamilishwa mwanzoni mwa msimu wa joto kati ya nchi hiyo, Uturuki na Russia, na kuwezesha kusafirishwa nafaka na mbolea ya Ukraine kupitia bandari kadhaa zilizokuwa zimewekewa mzingiro.Wawakilishi wa Uturuki, Umoja wa Mataifa, Russia na Ukraine walitia saini makubaliano hayo mjini Istanbul, Uturuki Julai 22, 2022.../


342/